Ijumaa, 29 Aprili 2016

VITU VINAVYOHARIBU NGOZI ZETU
Ngozi zetu zimeundwa kwa chembe ndogo ndogo zinazoitwa seli, ambazo ni viumbe hai; yaani huzaliwa, hukua na kufa. Seli za zamani zinakufa na seli mpya zinazaliwa kila siku. Huu ni utaratibu wa kawaida na hutokea kila siku katika maisha yetu, na ni mwili wenyewe ndio unaoendesha na kusimamia utaratibu huu. Ukiacha huo utaratibu wa kawaida wa seli za ngozi kuzaliwa, kukua na kufa kuna vitu vingine kutoka kwenye mazingira ambavyo huathiri utaratibu huo na kupelekea kudhoofika au kufa kwa seli zetu. Vitu hivyo vikitokea kwa kiasi kidogo hudhoofisha seli zetu, lakini vikiondolewa seli zetu hujijenga upya na kurudia hali yao ya kawaida. Vikitokea kwa kiasi kikubwa au kuendelea kuwepo kwa muda mrefu huzidhoofisha zaidi seli zetu na kuziua kabisa.
Vitu hivyo ni
i. Msongo wa mawazo
ii. Jua kali
iii. Ukosefu wa mlo mzuri
iv. Kutokunywa maji ya kutosha
v. Kujichubua
vi. Umri mkubwa
vii. Uchafu
viii. Vipodozi visivyo salama
ix. Magonjwa na maambukizi
x. Kujeruhiwa
Matokeo yake ni ngozi kuharibika, kuwahi kuzeeka au kupoteza uzuri wake.
Tunaweza kutunza ngozi zetu ili ziwe nzuri na zidumu na uzuri wake kwa Kupumzisha mwili na akili zetu kiasi cha kutosha, kuepuka jua kali, kupata mlo kamili, kunywa maji ya kutosha, kutojichubua, Kusafisha vizuri ngozi zetu na kuondoa uchafu wote, Kutumia vipodozi bora na salama, Kuwa makini ili tusipate majeraha na kujikinga vizuri dhidi ya magonjwa na maambukizi.

Ndugu msomaji, sasa umeshajua; Chukua hatua.

PICHA ZA CHINI ZINAONESHA BAADHI YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA



Jumatano, 27 Aprili 2016

TATIZO LA MAFUTA MENGI USONI
Habari rafiki! Karibu leo tuzungumzie tatizo la mafuta mengi usoni.
Mafuta ni moja kati ya vitu muhimu sana katika ngozi zetu. Na chini ya ngozi zetu (ndani ya mwili) kuna mafuta mengi yamehifadhiwa na pia kuna seli ambazo kazi yake kubwa ni kutoa haya mafuta. Mafuta haya yana kazi kuu kama mbili hivi:
Kwanza ni kutusaidia wakati wa baridi. Yanazuia joto kupotea na hutumika kuongeza joto la mwili
Pili yanasaidia kuipakaa ngozi na kuikinga dhidi ya maji kupotea na ngozi kusinyaa au kukauka. Kwa maana hii mafuta husaidia kuzifanya ngozi zetu kuwa nzuri na afya nzuri. Ngozi yenye mafuta mengi huwa na faida ya kutowahi kuzeeka, kutokauka, kutopata maambukizi kiurahisi na kutohitaji mafuta mengi ya kuongezea kwa ajili ya kuitunza.
TATIZO LA MAFUTA MENGI



Mafuta yakiwa ya wastani maisha yanakuwa mazuri pia na ngozi inaweza kukubali vipodozi mbalimbali vya kuongezea uzuri na urembo wa ngozi.
Mafuta yakiwa mengi yanaweza kushindwa kutoka vizuri wakati wa kuletwa nje ya ngozi na hivyo kukwama kutokana na kuzibwa kwa ngozi na uchafu au seli zilizokufa, matokeo yake ni kumletea mtu chunusi. Mara nyingi watu wenye mafuta mengi usoni wanakabiliwa na tatizo la chunusi na upele mwingine.
Inawezekana mtu akawa na asili tu ya kuwa na mafuta mengi, au yakaanza kuzalishwa kwa wingi kutokana na vipodozi anavyotumia kama vile scrub na vipodozi vingine ambavyo vitaifanya ngozi ihisi mafuta yamepungua kwenye uso wa ngozi na hivyo kuanza kuzalisha na kutoa mafuta mengi zaidi kuja nje ya ngozi.
USHAURI NA KUKABILIANA NA TATIZO LA MAFUTA MENGI USONI
Kama una mafuta mengi usoni ni faida sana kwako, kwa kuwa ngozi yenye mafuta mengi huwa na faida ya kutowahi kuzeeka, kutokauka, kutopata maambukizi kiurahisi na kutohitaji mafuta mengi ya kuongezea kwa ajili ya kuitunza.
Kama yanakusumbua kwa kujaa zaidi, kukuletea chunusi na matatizo mengine basi unaweza kuwa unayaosha kwa maji au kuyafuta kwa kitambaa kisafi na laini.
Kwa upande wa ushauri,
Kwanza tumia vipodozi (Lotion, Cream na Mafuta) ambavyo ni maalum kwa ajili ya ngozi za mafuta. Mara nyingi utakuta vimeandikwa FOR OILY SKIN au KWA NGOZI YA MAFUTA




Pili epuka scrub au itumie kwa ufundi ili isikusababishie mafuta mengi zaidi kuzalishwa na kukuzidishia chunusi. Hakikisha unapaka moisturiser nzuri kila baada ya kuscrub ili kuifanya ngozi yako isihisi ukavu na isizalishe mafuta mengine mengi zaidi
Tatu unaweza ukatumia poda na sabuni zinazosaidia kupunguza mafuta usoni. Mifano ni poda ya POND'S ile iliyoandikwa OIL CONTROL na sabuni za DOVE na PEARS zilizoandikwa OIL CONTROL SOAP

Nne usipasue chunusi yoyote kama nazo zitakuwepo. Kupasua chunusi kutakuachia makovu na madoa madogo madogo ambayo yatakuharibia uso wako.

Tano unashauriwa kutumia facial cleanser/face wash ili kuweza kuondoa uchafu, seli zilizokufa na mafuta yaliyoziba matundu.
Usifadhaike na ngozi yenye mafuta, ni nzuri. Ishi nayo vizuri.
Pia unaweza kuonana au kuwasiliana na wataalam na washauri wa afya, uzuri na vipodozi kwa ushauri na maelezo zaidi
S&E BEAUTY SOLUTIONS
WATAALAM NA WASHAURI WA AFYA, UREMBO NA VIPODOZI
0 659 528 724 au 0 784 082 847
Facebook : S&E BEAUTY SOLUTIONS

Jumatatu, 25 Aprili 2016

BAADA YA KUTUMIA VIPODOZI (LOTION, CREAM, MAFUTA NK) PUMZISHA NGOZI YAKO
Unashauriwa kuosha ngozi yako na kuondoa vipodozi vyako vyote (lotion, mafuta, cream nk) na kuiacha ngozi yako ikiwa free ili iweze kupumzika na kupumua vizuri. Osha kabisa vipodozi na uchafu wote utoke usoni au sehemu nyingine ya ngozi kisha baki hivyo kwa angalau masaa 6 kwa siku, either masaa 6 mfululizo au masaa 3 kutwa mara 2.
Ngozi yako itapata muda wa kupumua vizuri, kupumzika na kujijenga vizuri zaidi.
S&E Beauty Solutions inakutakia kila la kheri katika matunzo na uzuri wa ngozi yako
Ujumbe huu umeletwa kwako na
S&E Beauty Solutions
Wataalam na washauri wa Afya, Urembo Na Vipodozi
0 659 528 724 , 0 784 082 847

Jumapili, 24 Aprili 2016

KUJIPENDEZESHA SAWA, KUJIHARIBU HAPANA!

  KUJIPENDEZESHA SAWA, KUJIHARIBU HAPANA !

Unaendeleaje rafiki? Karibu kwenye somo la leo la kukushauri kujipendezesha na kukushauri kutokujiharibu kwa kupitia vipodozi unavyotumia.
Ni haki na ni vizuri kujipendezesha na kuwa na muonekano mzuri kwani muonekano wako ni sehemu ya moyo na maisha yako. Ukiwa na muonekano mzuri utachukuliwa kama ni mtu wa kuheshimiwa, kupendwa na kuthaminiwa. Ukiwa na muonekano mbaya inakuwa kinyume chake, labda uwe na vitu vingine vya kipekee sana.

VIPODOZI VYA KUTUMIA ILI KUJIPENDEZESHA VIZURI
Ukitaka kujipendezesha vizuri unashauriwa kuujua vizuri mwili wako (ngozi, kucha, nywele nk) ili utumie vipodozi vinavyoendana nao na malengo yako
Kama ni ngozi ni lazima ujue aina ya ngozi yako (Ngozi kavu, Ngozi ya mafuta, Ngozi ya kawaida au Ngozi mchanganyiko) ili utumie bidhaa zinazoendana na ngozi yako
Pia chagua maduka ya kuaminika kwa ajili ya kupata vipodozi vyako. Maduka mengine wanakuwa wanauza na vipodozi feki, visivyosajiliwa, vyenye sumu, vilivyopigwa marufuku, vilivyoharibika au kupita muda wake wa matumizi na kadhalika. Epuka sana kutumia vipodozi hivyo na hata kununua vipodozi kutoka kwenye maduka hayo
Chagua vipodozi vyenye ubora mzuri na ufanisi mzuri na vinavyopatikana kwa bei unayoimudu ili uweze kuvitumia vizuri na kwa uhuru bila kuathiri uchumi wako
Pata ushauri wa kitaalam kabla ya kuanza kutumia vipodozi usivyovijua. Mwambie unachohitaji kwenye mwili wako ili yeye akushauri vipodozi vya kutumia

VIPODOZI VITAKAVYOHARIBU MWILI WAKO



Usipotumia vipodozi vizuri unaweza ukapata madhara mengi na makubwa. Machache kati ya hayo ni kansa ya ngozi, maini, ubongo, mapafu na mfumo wa damu; ngozi kuungua, ngozi kuwasha sana, upofu, upotevu wa fahamu wa mara kwa mara, uziwi, kuumwa kichwa, kizunguzungu, fangasi na magonjwa mengine kwenye ngozi, aleji (mzio) ya ngozi, kuchubuka kwa ngozi, mabaka mabaka, chunusi kubwa kubwa, ngozi kuwa nyembemba sana na laini kiasi cha kidonda kuchelewa au kushindwa kupona endapo utapata jeraha au kufanyiwa operesheni na mengineyo mengi.
Vipodozi vitakavyokuharibu ni vile ambavyo
i.                    Haviendani na ngozi au mwili wako
Kwa mfano mtu mwenye uso au ngozi ya mafuta akitumia kipodozi kwa ajili ya ngozi kavu basi inaweza kumletea chunusi nyingi na matatizo mengine. Usitumie kipodozi chochote ambacho sio kwa ajili ya aina ya ngozi au mwili wako
ii.                  Vina kemikali ambazo ni sumu na hudhuru mwili wa binadamu na viungo vyake
Mifano ni Mercury (Zebaki), Hydroquinone na Betamethasone
iii.                Vimeharibika au muda wake wa matumizi umeisha. Hivi vinakuwa havina garantii ya ubora, ufanisi wala usalama
Hivi navyo ni hatari kwa afya yako, usivitumie.
iv.                Vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku, havijaidhinishwa na kusajiliwa na Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Tanzania (TFDA)
Hivi navyo havina garantii ya ubora, ufanisi wala usalama. Usivitumie.
v.                  Matumizi yake hayaendani na mahitaji yako
Ni vyema kuvielewa vizuri vipodozi au kupata ushauri wa vipodozi vya kutumia kulingana na matatizo au mahitaji yako. Usitumie vipodozi ambavyo haviendani na tatizo au hitaji lako, maana utakosa matokeo unayoyahitaji, utapoteza pesa, muda na vinaweza kukuletea matatizo mengine ambayo haukuwa nayo.

KUJIPENDEZESHA SAWA, KUJIHARIBU HAPANA!
Tunakushauri usitumie kipodozi chochote ambacho sio salama hata kama kinakuletea matokeo mazuri kwa haraka. Matatizo mengi ya vipodozi visivyo salama huwa ni makubwa na hayatibiki kirahisi, na mengine yanaua au kukupa ulemavu wa kudumu. Yanaweza kuja haraka au pole pole, kwa hiyo hata kama hauyaoini kwa sasa basi baadae yatafika.
Furahia ujana, furahia uzee. Vipodozi vibaya vinaweza vikakuzeesha haraka na kukupa matatizo mengi sana baadae na uzeeni.
Onana na wataalam wa urembo na vipodozi, pata ushauri.
Kwa maelezo zaidi na ushauri juu ya vipodozi na kupendezesha mwili wako wasiliana na wataalam

Ujumbe huu umeletwa kwako na wataalam na washauri wa Afya, Urembo na Vipodozi
S&E BEAUTY SOLUTIONS
TEMEKE BUZA NA ILALA BUNGONI
DAR ES SALAAM
Simu : 0 659 528 724 au 0 784 082 847

Kurasa za Facebook :          S&E BEAUTY SOLUTIONS
                          Na                 MSHAURI WA AFYA
                                  





                                  KUJIPENDEZESHA SAWA, KUJIHARIBU HAPANA !

Jumamosi, 23 Aprili 2016

TUMIA FACE WASH AU FACIAL CLEANSER KWA AJILI YA KUSAFISHA NA KUNG'ARISHA USO WAKO VIZURI ZAIDI

UTUMIAJI WA FACE WASH AU FACIAL CLEANSERS HUPENDEZESHA ZAIDI USO WAKO
U hali gani rafiki yetu na mpenzi wa mambo ya vipodozi na muonekano wa mwili? Karibu katika somo la leo linalohusiana na vipodozi viitwavyo Face Wash au Facial Cleanser vitumikavyo kwa ajili ya kuoshea uso.

FACE WASH/FACIAL CLEANSER NI NINI?
Face wash au Facial cleanser ni vipodozi vinavyofanya kazi ya kusafisha uso kwa kiasi kikubwa kabisa kwa kuyayusha na kuondoa kiasi kikubwa cha uchafu wa usoni kama vile mafuta, jasho, vumbi, seli zilizokufa na takataka zingine.
Matokeo yake ni kwamba mtu ambaye ametumia kipodozi hiki anabaki na ngozi safi kabisa na inayong’aa kwa sababu kiasi kikubwa sana cha uchafu na vitu vingine vilivyokuwa vinafunika ngozi yake vimeondolewa. Ufanisi wake katika kusafisha uso ni mkubwa kuliko sabuni.

KWA NINI NI BORA UKATUMIA FACE WASH AU FACIAL CLEANSER?
Kwanza Face wash au Facial cleanser zinasaidia kuondoa sehemu kubwa sana ya uchafu na vitu vingine vinavyoziba ngozi yako. Hii ni bora zaidi kwa sababu itakuacha na ngozi laini, inayong’aa na kuvutia vizuri.
Pili Face wash sio kali sana kama sabuni, na ni nzuri zaidi kuoshea uso wako. Sabuni huweza kuwa kali na pia kama ni ya mche au kipande huweza kuwa inaharibu ngozi yako na kupasua chunusi, kuleta michubuko nk kama utajisugulia kwa nguvu.
Hayo hufanya Face wash au Facial Cleansers kuwa bora zaidi katika kusaidia kuondoa chunusi na pimples, kung’arisha uso,  kumaliza uchafu usoni, kuzuia magonjwa ya ngozi usoni, kupunguza kasi ya uso kuzeeka na kuzipa seli za uso kuweza kupumua, kukua na kuendelea vizuri.

MAMBO YA KUZINGATIA
Chagua Face Wash/Facial Cleanser nzuri na yenye ubora unaofaa kwa ngozi yako. Kama ngozi yako ni kavu chagua Face wash kwa ajili ya ngozi kavu, na kama uso wako ni wa mafuta basi chagua face wash/facial cleanser kwa ajili ya uso wa mafuta. Kadhalika na kwa ngozi ya kawaida na ngozi mchanganyiko.
 Tafuta ya gharama unayoimudu vizuri ili uweze kuitumia vizuri na kwa uhuru zaidi.
Kuna Face wash/Facial Cleanser zinazoweza kuwa feki na kali kwa ngozi yako. Pata ushauri kutoka kwa watu wanaojua vizuri masuala ya vipodozi na uzuri wa mwili.

S&E BEAUTY SOLUTIONS inakutakia kila la kheri katika kujipendezesha na uzuri wako.
Kama una tatizo lolote , swali au unahitaji bidhaa yoyote au ushauri wa afya, urembo na vipodozi karibu sana kwetu.

S&E BEAUTY SOLUTIONS
TEMEKE BUZA NA ILALA BUNGONI
DAR ES SALAAM
Simu : 0 659 528 724 , 0 784 082 847
Au tembelea ukurasa wetu wa facebook uitwao S&E BEAUTY SOLUTIONS

Jumatano, 20 Aprili 2016

KUZEEKA KWA NGOZI ZETU NA JINSI YA KUPUNGUZA KASI YA KUZEEKA

JINSI YA KUIFANYA NGOZI YAKO KUWA CHANGA NA KUPUNGUZA KUZEEKA

KUZEEKA KWA NGOZI NA JINSI YA KUPUNGUZA KUZEEKA
Kuzeeka ni utaratibu wa kawaida kwa mwili wa binadamu. Na hutokea kila siku kwa yeyote ambaye ameshafika umri wa utu uzima. Hakuna shida yoyote kwa mtu kuwa mzee isipokuwa kama mtu anapenda au anahitaji muonekano wa ujana – ngozi laini, nywele nyeusi nk

JINSI KUZEEKA KWA NGOZI KUNAVYOTOKEA
Kuzeeka kunatokana na kuharibika na kupungua kwa protini za ngozi zinazofanya kazi ya kuifanya ngozi iweze kukua, kuvutika na kutunza maji ya kutosha. Protini hizi huitwa elastin na collagen.
Protini hizo zikiharibika na kupungua ngozi hushindwa kukua, hushindwa kuvutika na hupoteza maji na matokeo yake huanza kufubaa, kuwa ngumu na kuwa makunyanzi.
Pia kushindwa kuvutika kwa ngozi ndio sababu ya mtu kuwa na michirizi.

JINSI YA KUPUNGUZA AU KUONDOA KUZEEKA KWA NGOZI
Kuzeeka kwa ngozi kunaweza kupunguzwa au kuondolewa kwa kuongeza uzalishaji na kiasi cha protini aina za elastin na collagen
Hilo linaweza kufanikishwa kwa vipodozi vya aina mbalimbali katika mfumo wa lotion, cream, mafuta na kadhalika
Hizi zitasaidia kuifanya ngozi kuwa changa na ya kuvutia kwa kuisaidia kukua, kuvutika na kutunza maji ya kutosha.

VITU GANI UTUMIE KUFANIKISHA HILI
Kuna bidhaa za aina nyingi na za kampuni mbalimbali za kuweza kufanikisha zoezi hili. Mfano wa kwanza ni vipodozi vyenye Vitamin A au mazao yanayotokana na Vitamin A (Lazima upate ushauri wa kitaalam ndipo uanze kutumia na zikusaidie vizuri)
Pia kuna vipodozi vyenye Vitamin E. Hivi navyo husaidia sana kuifanya ngozi kuwa laini na ya kupendeza, na kupunguza kuzeeka kwa ngozi.
Kitu cha muhimu ni kusaidia kuondoa ngozi iliyozeeka, kuongeza uzalishaji wa elastin na collagen na kuongeza maji na utunzaji maji katika ngozi (Moisturizer husaidia kukamilisha zoezi la kuongeza maji katika ngozi. Chagua iliyo bora kabisa na utumie).
Pia kunaweza kuwa na tofauti ya mahitaji ya bidhaa kati ya mtu na mtu, kwa hiyo ni vyema kila mtu kushauriwa kutokana na ngozi yake na mahitaji yake.
EPUKA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILE VISIVYOFAA KWA NGOZI YAKO. VINAWEZA VIKAKUHARIBU ZAIDI.

PATA USHAURI WA KITAALAM, BIDHAA BORA NA SALAMA NA MAELEZO ZAIDI
Kwa kupata maelezo zaidi, ushauri wa kitaalam na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na usalama unaweza kuwasiliana na Washauri wa afya na wataalam wa urembo na vipodozi - S&E BEAUTY SOLUTIONS

S&E BEAUTY SOLUTIONS
TEMEKE BUZA BLOCK T PLOT No. 601
MASHINE YA MAJI NAMBA 5
DAR ES SALAAM
Simu : 0 659 528 724 , 0 784 082 847
Pia unaweza ukatembelea ukurasa wetu wa Facebook : S&E BEAUTY SOLUTIONS
E-mail : tecetra@gmail.com