Jumapili, 20 Machi 2016

Madhara ya kutumia GENTRISONE CREAM, SONADERM CREAM, MEDIVEN CREAM, BETASON CREAM na CORTICOSTEROIDS zingine kama vipodozi
Kuna kundi la kemikali linaitwa STEROIDS. Kundi hili linajumuisha dawa kama vile Hydrocortisone, Betamethasone, Beclometasone, Clobetasol, Dexamethasone nk
Kimsingi hizi ni dawa za allergy na husaidia kupunguza nguvu za kinga ya mwili.
Zinapokuwa katika mfumo wa cream, lotion au gel huweza kupakwa kwenye ngozi na kusaidia kuondoa allergy kwenye ngozi. Mbali na kuondoa allergy dawa hizi huondoa ngozi ngumu na rough ya nje (Ngozi ambayo hutusaidia kutukinga dhidi ya miale mikali ya jua, kansa, michubuko nk), hivyo kuiacha ngozi laini ya ndani kidogo ambayo haiwezi kutukinga vizuri dhidi ya miale mikali ya jua, kansa, michubuko nk.
Matokeo yake ni kupata matatizo ya ngozi kama vile muwasho, upele,majeraha kwa urahisi, kupunguza kinga ya mwili, magonjwa mengine ya ngozi na baadae kuweza kupata kansa ya ngozi.
JINSI YA KUJUA KAMA CREAM, LOTION AU GEL YAKO INA KEMIKALI HIZI
Angalia sehemu ya cream, gel au lotion yako walipoandika COMPOSITION au INGREDIENTS. Ukiona kwenye vilivyomo ndani kuna Beclomethasone, Betamethasone, Clobetasol, Dexamethasone, Hydrocortisone au Prednisolone basi jua kwamba unatumia STEROID.
MATUMIZI SAHIHI YA STEROIDS (CREAMS)
Steroids (Hydrocortisone, Betamethasone, Beclomethasone, Clobetasol, Dexamethasone nk) ni mahususi kwa ajili ya allergy tu za kwenye ngozi, kwa mfano kutibu muwasho, vipele na maumivu yatokanayo na kung'atwa na wadudu.
Mara nyingi matumizi yake inabidi yaanzishwe na mtaalam wa afya, hususan daktari.
Pia mara nyingi matumizi yake yasizidi wiki mbili. Maana baada ya hapo ndipo madhara yake yanaanza kujiandaa na kujitokeza.
USHAURI WA KITAALAM
Mshauri wa afya ninakushauri kuacha kutumia dawa hizi kama vipodozi mara moja. Na utumie kwa sababu za matibabu ya allergy ya ngozi tu, tena baada ya kushauriwa na mtaalam wa afya.
Kuna kundi kubwa sana la watu hususan wanawake, umri kuanzia miaka 16 hadi miaka 45 ambao wanatumia vipodozi hivi kila siku kwa ajili ya kufanya ngozi zao kuwa laini na nyororo. HII NI HATARI SANA!
Kuna vipodozi vingi vinavyoweza kumfanya mtu kuwa na ngozi nyororo na ya kuvutia bila kumletea madhara kwa afya yake.
unaweza kuwasiliana na washauri wa afya (AFYA ZAIDI CONSULTANTS - wapigie kwa 0659528724 au 0784082847) ukashauriwa juu ya vipodozi vizuri na salama vya kutumia kwa ajili ya kuwa na ngozi laini na ya kupendeza.
JIKINGE DHIDI YA MADHARA YATOKANAYO NA VIPODOZI HATARI
Acha matumizi ya STEROIDS kama vipodozi.
Pia pata ushauri wa kitaalam kutoka kwa wataalam wa afya na urembo ili uweze kupendeza bila kupata madhara yoyote.
Karibu sana kwa wataalam
S&E BEAUTY SOLUTIONS
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS
0659528724 na 0784082847
Pendeza Zaidi. Kuwa na Afya Zaidi.


Maoni 6 :

  1. Ni elimu nzuri sana, kwani imefanya nijue kwamba kumbe hizi cream zina muda wake wa matumizi ambayo ni wiki mbili tu. Asante sana

    JibuFuta
  2. Betasol pekee yake ina madhara?

    JibuFuta
  3. jamani naomba ushauri mediven mafuta kwani nayo ina madhara?

    JibuFuta
  4. Mi natumia skderm kwan nayenyewe inamazara

    JibuFuta
  5. Kuna tofauti gain Kati ya cream na ointiment?

    JibuFuta